Psalms 103:8-13

8 a Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9 bYeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10 cyeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11 dKama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;
12 ekama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13 fKama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;
Copyright information for SwhNEN